Kiende ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Waende kwenye kisiwa cha Flores. Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kiende imehesabiwa kuwa watu 110,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiende iko katika kundi la Kibima-Lembata.