Kiestonia

Kiestonia ni lugha ya Kifini-Kiugori nchini Estonia na Ufini inayozungumzwa na Waestonia. Ni lugha rasmi ya Estonia. Mwaka wa 2012 idadi ya wasemaji wa Kiestonia nchini Estonia imehesabiwa kuwa watu 1,040,000. Pia kuna wasemaji 33,100 nchini Ufini (2013).

Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiestonia iko katika kundi la Kifini. Wengine huangalia Kivõro kuwa lahaja ya Kiestonia badala ya lugha tofauti.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne