Kieuskara (au Kibaski) ni lugha hai ya pekee[1] inayotumiwa na Wabaski hasa mpakani mwa Hispania kaskazini na Ufaransa kusini-magharibi kwenye milima ya Pirenei karibu na bahari ya Atlantiki.[2]
Ingawa inakubalika ilikuwa inatumika huko kabla ya lugha za Kihindi-Kiulaya kuenea Ulaya magharibi, haieleweki ilianzaje, kwa sababu hakuna lugha yoyote inayofanana nayo.
Wanaoitumia ni kama watu 715,000, wengi wao wakiwa Hispania, ambako inalindwa na kustawishwa zaidi.