Kifas ni lugha ya Kipapua nchini Papua Guinea Mpya inazungumzwayo na Wafas. Mwaka wa 2000 idadi ya wazungumzaji wa Kifas imehesabiwa kuwa watu 2500. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kifas iko katika kundi lake lenyewe la Kifas. Lugha la pekee linalohusiana na Kifas ni Kibaibai.