Kigalolen

Kigalolen (pia Kiilwaki) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Timor-Mashariki na Indonesia inayozungumzwa na Wagalolen kwenye visiwa vya Timor na Wetar. Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kigalolen nchini Timor-Mashariki imehesabiwa kuwa watu 13,000. Pia kuna wasemaji 680 nchini Indonesia (1990). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigalolen iko katika kundi la Kitimor-Babar.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne