Kigidar

Kigidar ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Kamerun na Chad inayozungumzwa na Wagidar. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kigidar imehesabiwa kuwa watu 54,000. Pia mwaka wa 1993, wasemaji 11,700 wamehesabiwa nchini Chad. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigidar iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne