Kigogodala ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wagogodala. Mwaka wa 2004 idadi ya wasemaji wa Kigogodala imehesabiwa kuwa watu 22,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigogodala iko katika kundi lake lenyewe la Kigogodala.