Kigule ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Sudan iliyozungumzwa na Wagule. Mwaka wa 1983 idadi ya Wagule imehesabiwa kuwa watu 1000 tu lakini walikuwa wameshasahau lugha yao yaani hawakuendelea kuongea Kigule. Kwa hiyo, lugha ya Kigule imetoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigule iko katika kundi la Kikomuz.