Kiguliguli ilikuwa lugha ya Kiaustronesia nchini Visiwa vya Solomon iliyozungumzwa na Waguliguli. Kwa miaka mingi sasa hakuna wasemaji wa Kiguliguli, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiguliguli iko katika kundi la Kioseaniki.