Kihelong

Kihelong (pia Kisemau) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wahelong kwenye visiwa vya Semau na Timor. Mwaka wa 1997 idadi ya wasemaji wa Kihelong imehesabiwa kuwa watu 14,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kihelong iko katika kundi la Kitimor-Babar.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne