Kiibaloi

Kiibaloi ni lugha ya Kiaustronesia nchini Ufilipino inayozungumzwa na Waibaloi. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kiibaloi imehesabiwa kuwa watu 111,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiibaloi iko katika kundi la Kifilipino.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne