Kiidoma

Kiidoma ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Waidoma. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kiidoma imehesabiwa kuwa watu 600,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiidoma iko katika kundi la Kiidomoidi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne