Kiili'uun (pia Kierai) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Waili'uun kwenye visiwa vya Wetar na Lirang. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kiili'uun imehesabiwa kuwa watu 1400. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiili'uun iko katika kundi la Kitimor-Babar.