Kijahanka

Kijahanka ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Guinea inayozungumzwa na Wajahanka. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kijahanka imehesabiwa kuwa watu 12,600. Pia kuna wasemaji 500 nchini Mali. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kijahanka iko katika kundi la Kimande.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne