Kijorto

Kijorto ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Nigeria inayozungumzwa na Wajorto. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kijorto imehesabiwa kuwa watu 17,300. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kijorto iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne