Kikairui-Midiki

Kikairui-Midiki ni lugha ya Kiaustronesia nchini Timor ya Mashariki inayozungumzwa na Wakairui na Wamidiki. Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kikairui-Midiki imehesabiwa kuwa watu 15,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikairui-Midiki iko katika kundi la Kitimor-Babar.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne