Kikakwa

Kikakwa ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Uganda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Wakakwa. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kikakwa nchini Uganda imehesabiwa kuwa watu 130,000. Pia kuna wasemaji 40,000 nchini Sudan Kusini na 20,000 nchini Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikakwa iko katika kundi la Kinilotiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne