Kikamberau ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Indonesia inayozungumzwa na Wakamberau. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kikamberau imehesabiwa kuwa watu 1570. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikamberau iko katika kundi la Kisabakor.