Kikanuri ni jina la kundi la lugha za Kinilo-Sahara nchini Nigeria, Niger, Chad na Kamerun. Idadi ya wasemaji wa lugha zote za Kikanuri inakaribia watu milioni nne. Baadhi ya lugha za Kikanuri kuna Kikanuri ya Kati, Kikanuri-Manga na Kikanuri-Tumari. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikanuri kiko katika kundi la Kisahara la Mashariki.