Kikara (pia Kiregi) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wakara, wakazi wa kisiwa kimojawapo cha Ziwa Viktoria.
Mwaka 1987 idadi ya wasemaji wa Kikara ilihesabiwa kuwa watu 86,000.
Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikara iko katika kundi la E20. Inafanana na Kijita (81%) na Kikwaya (80%).