Kikasanga ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Guinea-Bisau inayozungumzwa na Wakasanga. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kikasanga imehesabiwa kuwa watu 690 tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikasanga iko katika kundi la Kiatlantiki.