Kike'o ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wake'o kwenye kisiwa cha Flores. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kike'o imehesabiwa kuwa watu 40,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kike'o iko katika kundi la Kibima-Lembata.