Kikera

Kikera ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Chad na Kamerun inayozungumzwa na Wakera. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kikera nchini Chad imehesabiwa kuwa watu 44,500. Pia kuna wasemaji 6000 nchini Kamerun. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikera iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne