Kikintaq ni lugha ya Kiaustro-Asiatiki nchini Malaysia inayozungumzwa na Wakintaq. Mwaka wa 2008 idadi ya wasemaji wa Kikintaq imehesabiwa kuwa watu 110 tu. Pia kuna angalao msemaji mmoja nchini Uthai (2007). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikintaq iko katika kundi la Kiaslian.