Kikiong ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Wakiong. Mwaka wa 2004 idadi ya wasemaji wa Kikiong imehesabiwa kuwa watu 100 tu. Kwa vile hasa ni wazee tu wanaoweza kuzungumza lugha ya Kikiong, lugha yao imekaribia kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikiong iko katika kundi la Cross River.