Kikota ni lugha ya Kibantu nchini Gabon na Jamhuri ya Kongo inayozungumzwa na Wakota. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kikota nchini Gabon imehesabiwa kuwa watu 34,400. Pia kuna wasemaji zaidi ya 9000 nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikota iko katika kundi la B20.