Kilari (pia Kilaari) ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kongo na Angola inayozungumzwa na Walari. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kilari nchini Kongo imehesabiwa kuwa watu 90,600. Idadi ya wasemaji nchini Angola ni ndogo zaidi isiyojulikana hasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kilari iko katika kundi la H10.