Kilele ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Walele. Isichanganywe na lugha ya Kilele nchini Chad. Mwaka wa 1971 idadi ya wasemaji wa Kilele imehesabiwa kuwa watu 26,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kilele iko katika kundi la C90.