Kilema Kusini ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,815 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22,711 [2] walioishi humo.
Msimbo wa posta ni 25226.
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Juda Thadaeus Ruwa'ichi, alizaliwa hapa mwaka 1954 katika kijiji cha Mulo.
Kilema pia ni sehemu inayotukuzika kihistoria kwani mche wa kwanza wa kahawa Tanzania ulioteshwa Kilema. Wenyeji wanaamini kuwa chimbuko la jina la mlima Kilimanjaro pia lilianzia Kilema. Watu walikuwa wakiuita mlima huo Kilema Kyaryo "yaani kilima cha kupanda" lakini wageni wakashindwa kutamka na kusema Kilimanjaro.