Kilifi | |
Mahali pa mji wa Kilifi katika Kenya |
|
Majiranukta: 3°38′0″S 39°51′0″E / 3.63333°S 39.85000°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Kilifi |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 122,899 |
Kilifi ni mji kwenye pwani ya kusini ya Kenya uliopo kati ya Mombasa na Malindi. Iko kando ya kihori cha Kilifi ("Kilifi Creek") kinachoishia katika Bahari Hindi.
Mji ni makao makuu ya Kaunti ya Kilifi.
Wakati wa sensa ya mwaka 2009 Kilifi ilikuwa na wakazi 122,899 [1].
Kilifi imekuwa kitovu kimojawapo cha utalii nchini Kenya hasa kutokana na fuko zake za kupendeza na Bofa Beach ni marufuku hasa. Mdomo mpana wa kihori unapendwa na wenye jahazi za burudani, hivyo kuna jahazi nyingi zinazolala hapa.