Kilimbum ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Walimbum. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kilimbum imehesabiwa kuwa watu 73,000. Pia kuna wasemaji nchini Nigeria. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilimbum iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.