Kilomita ya mraba

Kilomita ya mraba (km²) ni kipimo cha eneo; eneo lenye upana na urefu wa kilomita moja

Msingi wake ni mita ya mraba (m²). Kilomita ya mraba hutumika kwa upimaji wa maeneo makubwa duniani kama mji, mkoa, nchi au dunia yote.

Kilometa 1 ya mraba (km²) ni sawa na:

  • eneo la mraba yenye urefu wa kilomita moja kila upande
  • Mita ya mraba 1,000,000
  • Hektari 100
  • Ekari 247.105 381
  • Maili ya mraba 0.386 102

Au:

  • Mita ya mraba 1 = kilometa ya mraba (km²) 0.000 001
  • Hektari 1= kilometa ya mraba (km²) 0.01
  • Maili ya mraba 1 = kilometa ya mraba 2.589 988
  • Ekari 1 = kilometa ya mraba 0.004 047

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne