Kiluchazi

Kiluchazi ni lugha ya Kibantu nchini Angola inayozungumzwa na Waluchazi. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kiluchazi nchini Angola imehesabiwa kuwa watu 155,000. Pia kuna wasemaji wa Kiluchazi nchi za Namibia na Zambia (54,400 - 1986). Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiluchazi iko katika kundi la K20.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne