Kima'di ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Uganda inayozungumzwa na Wama'di. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kima'di nchini Uganda imehesabiwa kuwa watu 296,000 (idadi hii imeaminika kuwa pamoja na wasemaji wa Kima'di ya Kusini ambacho ni lugha tofauti). Pia kuna wasemaji 18,000 nchini Sudan Kusini. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kima'di iko katika kundi la Kimoru-Madi.