Kimaba (pia Kibicoli) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wamaba kwenye kisiwa cha Halmahera. Isichanganywe na lugha ya Kimaba izungumzwayo nchini Chad. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimaba imehesabiwa kuwa watu 6620. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimaba iko katika kundi la Kihalmahera-Kusini.