Kimakhuwa-Moniga ni lugha ya Kibantu nchini Msumbiji inayozungumzwa na Wamakua. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kimakhuwa-Moniga imehesabiwa kuwa watu 200,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimakhuwa-Moniga iko katika kundi la P30.