Kimalay cha Baba

Kimalay ya Baba ni lugha ya Kiaustronesia nchini Singapuri na Malaysia inayozungumzwa na Wamalay. Mwaka wa 1986 idadi ya wasemaji wa Kimalay ya Baba nchini Singapuri imehesabiwa kuwa watu 10,000. Pia kuna wasemaji 2000 nchini Malaysia (2006). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimalay ya Baba iko katika kundi la Kimalayiki. Wengine huiangalia kama krioli.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne