Kimangarayi ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wamangarayi katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kimangarayi ilihesabiwa kuwa watu kumi na watano tu, yaani lugha iko hatarini mwa kutoweka. Uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi haujulikani kwa uhakika.