Kimaninka-Misitu ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Cote d'Ivoire inayozungumzwa na Wamaninka. Idadi ya wasemaji wa Kimaninka-Misitu imehesabiwa kuwa watu 15,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimaninka-Misitu iko katika kundi la Kimande.