Kimankanya

Kimankanya ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Guinea-Bisau, Senegal na Gambia inayozungumzwa na Wamankanya. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kimankanya imehesabiwa kuwa watu 44,200 nchini Guinea-Bisau, na 29,200 nchini Senegal. Pia kuna awsemaji wachache nchini Gambia. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimankanya iko katika kundi la Kiatlantiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne