Kimanusela (pia Kiwahai) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wamanusela kwenye kisiwa cha Seram. Mwaka wa 1989 idadi ya wasemaji wa Kimanusela imehesabiwa kuwa watu 7000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimanusela iko katika kundi la Kimaluku.