Kimarma

Kimarma ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Bangladesh na Uhindi inayozungumzwa na Wamarma. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kimarma nchini Bangladesh imehesabiwa kuwa watu 150,000. Pia kuna wasemaji 30,600 nchini Uhindi (2001). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kimarma iko katika kundi la Kingwi-Burma. Wengine huiangalia kuwa sawa na lugha ya Kirakhine nchini Myanmar.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne