Kimarovo

Kimarovo ni lugha ya Kiaustronesia nchini Visiwa vya Solomon inayozungumzwa na Wamarovo kwenye visiwa vya Georgia Mpya, Vangunu na Nggatokae. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kimarovo imehesabiwa kuwa watu 8090. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimarovo iko katika kundi la Kioseaniki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne