Kimaslam

Kimaslam ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Kamerun inayozungumzwa na Wamaslam. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kimaslam imehesabiwa kuwa watu 250 tu. Pia kuna wasemaji wachache sana nchini Chad. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimaslam iko katika kundi la Kichadiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne