Kimbo ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Wambo. Mwaka wa 1994 idadi ya wasemaji wa Kimbo imehesabiwa kuwa watu 11,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimbo iko katika kundi la D30.