Kimoba

Kimoba ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Togo inayozungumzwa na Wamoba. Isichanganywe na Kibimoba cha Ghana; ingawa lugha hizo mbili zinafanana, hazielewekani. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kimoba imehesabiwa kuwa watu 189,000. Pia kuna wasemaji 1800 nchini Burkina Faso. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimoba iko katika kundi la Kigur.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne