Kimoikodi ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wamoikodi. Mwaka wa 1981 idadi ya wasemaji wa Kimoikodi imehesabiwa kuwa watu 570. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimoikodi iko katika kundi la Kiyareban.