Kimongol

Kimongol ni lugha ya Kipapua nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wamongol. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kimongol imehesabiwa kuwa watu 340. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kimongol iko katika kundi la Kimongol-Langam, na inahusiana na lugha mbili nyingine tu, Kilangam na Kiyaul.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne