Kimungaka

Kimungaka ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wamungaka. Mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kimungaka imehesabiwa kuwa watu 50,100. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimungaka iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne