Kimurrinh-Patta ni lugha ya Kidaly nchini Australia inayozungumzwa na Wamurrinh-Patta katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kimurrinh-Patta 1,800, na lugha imekuwa lugha ya mawasiliano katika eneo la Wadeye jimboni mwa Northern Territory. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimurrinh-Patta kiko katika kundi lake lenyewe la Kimurrinhpatta.